Watu 494 wamekutwa na virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita baada ya sampuli 6,428 kupimwa na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 166,876.

Katika taarifa, Waziri wa afya Mutahi Kagwe ametangaza kuwa watu 50 zaidi wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 114, 285 huku maafa 5 zaidi yakidhibitishwa na kufikisha idadi hiyo kuwa  3,040.

Maambukizi ya ugonjwa huo nchini kwa sasa yako katika asilimia 7.7%.

Kuhusu shughuli ya utoaji chanjo ya ya virusi vya corona inayoendelea kote nchini, waziri Kagwe ametangaza kuwa jumla ya watu 948, 980 wamepata chanjo hiyo ikiwemo wahudumu wa afya 163, 490, waalimu 149, 018, maafisa wa usalama 80, 153.