Mtoto wa siku mbili ni miongoni mwa watu 376  waliambukizwa virusi vya korona  baada ya kupima sampuli 4,153  katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Hii ina inafikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 166,382.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amedhibitiska kupona kwa watu 318 zaidi na kufikisha jumla ya idadi ya waliopona kuwa 117,235.

Wagonjwa wengine 14 wamefariki na kufikisha idadi ya maafa kuwa 3,035.

Kufikia sasa watu 945,597  wamepata chanjo ya virusi vya corona.