Aliyekuwa Gavana wa Wajir Mohamed Abdi Mohamud amelalamikia kile anasema ni kupuuzwa kwa agizo la mahakama baada ya naibu wake Ahmed Ali Muktar kuapishwa kumrithi.
Kupitia kwa wakili wake Ndegwa Njiru, Gavana huyo anasema mahakama kuu ilifutilia mbali kutimuliwa kwake na bunge la seneti hadi pale kesi aliyowasilisha itakaposkizwa na kuamuliwa.
Gavana huyo anamtuhumu msajili mkuu wa mahakama Anne Amadi kwa kuidhinisha kuapishwa kwa Gavana Muktar licha ya kuwepo kwa agizo la mahakama.
Muktar aliapishwa jana kuwa Gavana mpya wa Wajir baada ya kutimuliwa kwa Mohamud na bunge la seneti.
Katika hotuba yake baada ya kuapishwa, Muktar ameahidi kuyapa kipaumbele masuala yanayoawathiri wakaazi wa Wajir moja kwa moja ikiwemo kuwawezesha kupata maji safi na pia elimu.