Wapiga kura katika maenoebunge ya Juja na Nyaribari Chache katika kaunti za Kiambu na Kisii mtawalia wanaelekea debeni hii leo kuchagua wabunge wao.

Tume ya uchaguzi IEBC imesema kila kitu ki shwari na tayari vituo vya kupigia kura vimefunguliwa.

Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati anasema wapiga kura ambao hawatakuwa na barakoa hawataruhusiwa kushiriki zoezi hilo.

Viti hivyo vilisalia wazi kufuatia kufariki kwa wabunge Francis Munyua Waititu na John Oroo Oyioka mtawalia.

Katika wadi ya Bonchari, zaidi ya wawaniaji kumi wanangangania kiti hicho huku kivumbi kikitarajiwa kati ya Zebedeo Opore wa Jubilee, Pavel Oimeke wa ODM na mjane wa mwendazake Oyioka Teresa Bitutu anayepeperusha bendera ya chama cha United democratic Alliance UDA.

Katika eneobunge la Juja, kivumbi ni kati ya mjane wa marahemu Waititu Susan Waititu na George Koimburi wa chama cha Peoples Empowerment PDP ambacho kinaongozwa na mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria.

Vile vile tume hiyo hii leo inaandaa uchaguzi mdogo katika wadi ya Rurii kaunti ya Nyandarua.