Katika eneobunge la Juja kaunti ya Kiambu, idadi ndogo ya wapiga kura 114,761 waliosajiliwa imejitokeza kushiriki zoezi hilo.
Vituo vilifunguliwa saa kumi na mbili asubuhi na hadi kufikia sasa, foleni si ndefu ambazo zinashuhudiwa.
Maafisa wa tume ya uchaguzi katika eneobunge hilo wameelezea Imani yao kuwa idadi hiyo itaongezeka.
Awali, kulikuwa na kizaazaa katika kituo cha kupigia kura cha Magomano baada ya wananchi kudai kuwa gari ya polisi ilikuwa imebaba karatasi za kuiba kura, ila ilipofunguliwa wakapata ni barakoa.
Wawaniaji kumi na mmoja wanamenyana kumrithi marahemu Francis Wakapee, akiwemo mjane wa marahemu Susan Njeri Waititu wa Jubilee na George Ndungu Koimburi wa chama cha Peoples Empowerment PDP ambacho kinaongozwa na mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria.