Maambukizi ya ugonjwa ya corona nchini yameshuka na kufikia asilimia 3% baada ya watu 86 kukutwa na ugonjwa huo kati ya sampuli 2,789 zilizopimwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.
Mtoto wa miezi saba ni miongoni mwa waliopaawa na ugonjwa huo na kufikisha idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini kuwa 165,465 kwa mujibu ya waziri wa afya Mutahi Kagwe.
Idadi ya maafa vile vile imepungua watu 2 wakifariki katika muda huo na kufikisha idadi ya waliofariki kuwa 3,003 huku waliopona wakifikia 113,612 baada ya kupona kwa wagonjwa 123.