Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amekuwa kiongozi wa hivi punde kuwataka wenzake kuheshimu uamuzi wa mahakama uliosimamisha mchakato wa BBI.

Kalonzo ambaye amesema hakubaliani na uamuzi huo ametoa wito kwa viongozi kukoma kuwatusi majaji na badala yake kusubiri rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Makamu huyo wa rais wa zamani ambaye ameshauri kuwepo na subira amesadiki kwamba ni wakati wa kuirekebisha katiba kwa manufaa ya taifa nzima.

Wito kama huu wa kuheshimu mahakama umetolewa na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga, Musalia Mudavadi wa ANC na Moses Wetangula wa FORD K.