Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria ameliambia shirika la habari la BBC kwamba ni kawaida kwa wabunge kuhongwa ili kupitisha hoja au miswada inayofadhiliwa na serikali.

Kwa mfano, Kuria amedai kuwa walipewa hongo ya Sh100,000 kumuidhinisha Amos Kimunya kama kiongozi wa walio wengi kufuatia kufurushwa kwa Aden Duale.

Amesema yuko tayari kurudisha pesa hizo iwapo hilo litahitajika.

Kuria alikuwa anajibu maswali kuhusu madai ya kwamba baadhi ya wabunge walihongwa ili kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba BBI.

Mbunge huyo pamoja na wenzake Ndindi Nyoro (Kiharu) na Mohammed Ali (Nyali) wanatazamiwa kufika bunge alasiri ya leo kutoa mwanga zaidi kuhusu madai yao.