Bunge la kitaifa limemsaili Jaji Mkuu mteule Martha Koome huku akiahidi kuhakikisha kuwa asasi tatu kuu za serikali zinafanya kazi pamoja.

Akijibu maswali mbele ya kamati ya bunge kuhusu haki na sheria (JLAC), Koome anasema kuwa afisi ya rais, bunge na mahakama zinapaswa kushirikiana kwa makusudi ya kuboresha utoaji wa haki.

Na ili kushughulikia kwa haraka kesi za ufisadi, Koome amependekeza ushirikiano wa karibu baina baraza la kitaifa kuhusu haki pamoja na asasi za uchunguzi.

Kuhusu mrundiko wa kesi mahakamani, jaji Koome ameiambia kamati hiyo inayoongozwa na mbunge wa Kangema Muturi Kigano kwamba kunafaa kuwa na jopo la kusikiliza lalama ni muhimu katika kuwapa wakenya njia mbadala za kutatua mzozo na kuhakikisha kuwa kila mmoja anapata haki

Kamati ya JLAC inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake bungeni Mei 25 mwaka huu wa 2021.

Iwapo bunge litaidhinisha uteuzi wake, Koome atakuwa Jaji Mkuu wa kwanza mwanamke katika taifa la Kenya.