Kamati ya maseneta 11 iliyobuniwa kubaini hatma ya gavana wa Wajir Mohamed Mohamud Abdi inaanza vikao vyake leo.
Bunge la kaunti ya Wajir linatazamiwa kuwasilisha mashtaka dhidi ya gavana huyo kwa kamati hiyo chini ye uenyekiti wake seneta wa Nyamira Okong’o Omogeni.
Madiwani wa bunge hilo watawasilisha ushahidi kudhibitisha mashtaka dhidi ya gavana huyo ikiwemo matumizi mabaya ya mamlaka na ukiukaji wa katiba.
Kesho itakuwa ni zamu ya gavana Mohamud kujitetea kabla ya kamati hiyo kutayarisha ripoti itakayowasilishwa bungeni Jumatatu ijayo ambayo ni Mei 17.
Maseneta wengine kwenye kamati hiyo ni; Susan Kihika (Nakuru), Sakaja Johnson (Nairobi), Mwangi Githiomi (Nyandarua), Hargura Godana (Marsabit), Fredrick Outa (Kisumu), Agnes Muthama (Machakos), Issa Juma (Kwale), Mithika Linturi (Meru) na maseneta wateule Christine Zawadi na Petronilla Were.