Polisi wawili waliomuua kwa kumpiga risasi mwanamke mmoja City Park, Nairobi miaka miwili iliyopita wamekutwa na hatia ya muaji ya kutokusudia.

Wawili hao William Chirchir na Godfrey Kirui wamepatwa na hatia ya kumuua mfanyibiashara Janet Waiyaki mnamo Mei 20, 2018.

Polisi hao walimuua kwa kumpiga risasi mwanamke huyo aliyekuwa kwenye gari na binamuye Benard Chege.

Jaji wa mahakama kuu Stella Mutuku ameamuru kuwa polisi hao walitumia nguvu kupita kiasi ilhali mwanamke huyo hakuwa tishio kwa usalama wao.

Ameongeza kuwa marehemu hakuwa na kosa lolote na wala hapakuwa na tishio lolote lililosababishwa walipokuwa kwenye gari lao.