Spika wa bunge la Senate Ken Lusaka ameamuru kwamba maseneta hawana mamlaka ya kubadilisha mswada wa marekebisho ya katiba BBI.

Kwenye uamuzi wake, Lusaka sawa na mwenzake wa bunge la kitaifa Justine Muturi, ameelezea kwamba bunge hilo halina mamlaka ya kurekebisha mswada kama huo unaolenga kubadilisha katiba kupitia kwa kura ya maamuzi.

Spika Lusaka ameamuru kwamba jukumu la Senate kwenye mswada kama huo ni kuukataa au kuupitisha na wala sio kuurekebisha.

Maseneta Irungu Kang’ata (Murang’a), Enock Wambua (Kitui), Samson Cherargei (Nandi) na seneta mteule Milicent Omanga walikuwa wamewasilisha notisi wakitaka mswada huo kufanyiwa marekebisho.