Kenya imepiga marufuku safari za ndege kuingia na kutoka nchini Somalia.

Katika taarifa, mamlaka ya safari za angani KCAA imesema marufuku hiyo inaanza kutekelezwa mara moja.

Wanaoruhusiwa kuendelea na safari za kuingia na kutoka Somalia kuanzia sasa ni mashirika yanayotoa misaada ya kibinadamu na wahudumu wa Afya.

Hata hivyo serikali haijatoa taarifa yoyote kuhusiana na sababu za marufuku hiyo ambayo inajiri siku chache tu baada ya mataifa hayoa mawili kurejesha mahusiano yake ya kidiplomasia.

Kenya na Somalia zilizika mgogoro wa miezi mitano baada ya taifa la Qatar kuingilia kati.