Seneta mteule Isaac Mwaura amepoteza kiti cha baada ya kufukuzwa na chama tawala cha Jubilee.

Spika wa bunge la Senate Ken Lusaka ametangaza kupitia kwa gazeti rasmi la serikali kiti hicho kuwa wazi kuanzia Mei 7 mwaka huu wa 2021.

Mwaura amepoteza kiti chaka baada ya jopo la kutatua mizozo ya vyama vya kisiasa kuamuru kwamba chama chake cha Jubilee kilikuwa sawa kumfurusha kwa kuzingatia sheria za vyama vya kisiasa.

Jubilee ilimtimua Mwaura kwa misingi kwamba amekuwa akiuza sera za chama kingine kinyume na kanuni zinazolinda vyama vya kisiasa.