Hatma ya mchakato wa kuifanyia katiba marakebisho kupitia kwa mswada wa BBI itaamuliwa Alhamisi wiki hii.

Jopo la majaji watanao ambalo limekuwa likiskiliza kesi kutoka kwa walalamishi saba linatazamiwa kutoa uamuzi wake siku ya Alhamisi.

Walalamishi hao akiwemo mwanauchumi David Ndii, muungano wa wauguzi nchini KNUN, chama cha Thirdway Alliance, shirika la 254Hope na wakenya Justus JUma, Moraa Omoke, Isaac Aluochir na shirika la MUHURI wanapinga mchakato hao kwa madai kuwa unakiuka katiba.

Mwezi februari, majaji hao Joel Ngugi, George Odunga, Jarius Ngaah, Janet Mulwa na Chacha Mwita waliisimamisha tume ya uchaguzi IEBC kuendelea mbele na mipango ya kuandaa kura ya maamuzi.