Wanafunzi wameanza kurejea shuleni hii leo kwa muhula wa tatu ambao umechelewa kutokana na janga la corona.

Utafiti uliofanywa na kituo hiki umeonyesha kuwa wengi wa wazazi asubuhi hii wamekuwa na wanao wakiwapeleka shuleni.

Hata hivyo katika baadhi ya Baringo baadhi ya wanafunzi hawatarejea shuleni hii leo kutokana na utovu wa usalama katika baadhi ya maeneo.

Katika kaunti ya Nairobi, barabara kadhaa zimeshuhudia msongamano wa magari kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi wanaorejea shuleni.

Wakati uo huo,

Wanafunzi kumi na tano kutoka eneobunge la Gichugu kaunti ya Kirinyaga wanatazamiwa kufikishwa mahakamani hii leo.

Wanafunzi hao ikiwemo wasichana watatu walinaswa wakibugia vileo na kushiriki tendo la ndoa.

Mkuu wa polisi katika eneo hilo Anthony Mbogo anasema wanafunzi hao walitazamiwa kuripoti shuleni hii leo.

Wanafunzi hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kianyaga wakisubiri kufikishwa katika mahakama ya Gichugu.