Inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai amewahakikishia wakaazi wa eneo la Kapedo kuwa wanafanya kila wawezalo kupata suluhu la kudumu kwa utovu wa usalama eneo hilo.

Akijibu maswali ya wananchi kupitia kwa mtandao wa Twitter, Mutyambai anasema kwa sasa kuna mazungumzo ambayeoyanaendelea na jamii za eneo hilo ili kupata suluhu la suala tata ikiwemo wizi wa mifugo.

Mutyambai ameongeza kuwa kwa sasa, maafisa wake wako katika eneo hilo kuzuia mashambulizi ya kulipiza kisasi.