Rais Uhuru Kenyatta anasubiriwa kumuapisha rasmi William Ouko kuwa jaji wa mahakama ya upeo.

Tume ya huduma za mahakama (JSC) chini ya uenyekiti wake Profesa Olive Mugenda imemteua rais huyo wa mahakama ya rufaa baada ya kuwahoji watu saba waliotuma maombi kujaza nafasi hiyo iliyosalia wazi kufuatia kustaafu kwa jaji Jackton Ojwang’.

Jaji Ouko ambaye alijaribu bahati yake kuwa Jaji Mkuu ni miongoni mwa watu waliofunga ukurasa wa mahojiano hayo na aliiambia JSC kwamba kuna haja ya mahakama ya upeo kushughulikia kesi zinazohusiana na uchaguzi chini ya muda wa miezi sita badala ya kuchukua muda mrefu kuzishughulikia.

Wengine waliohojiwa kwa wadhifa huo ni; majaji Said Juma Chitembwe, Nduma Nderi, Njagi Marete,Joseph Sergon, msomi Dkt. Lumumba Nyaberi na wakili Alice Yano.