Spika wa bunge hilo Ken Lusaka anatazamiwa kutoa uamuzi kuhusu iwapo au la mswada wa marekebisho ya katiba BBI unafaa kufanyiwa marekebisho.

Hii ni baada ya maseneta kumtaka kutoa mwelekeo kuhusu ni vipi wataendelea na mjadala huo ilhali wenzao wamependekeza marakebisho kwenye mswada huo.

Seneta wa Uasin Gishu Profesa Margaret Kamar na mwenzake wa Busia Amos Wako wamependekeza mswada huo kupitishwa bila kuufanyia marekebisho.

Kwa upande wake seneta wa Kakamega Cleophas Malala ametaja bunge hilo linafaa kuufanyia mabadiliko kabla ya zoezi la kuupigia kura.