Dkt. Jamleck Muturi ameanza rasmi majukumu yake kama mwenyekiti mpya wa tume ya huduma za walimu TSC.

Muturi atakayehudumu kwa muda wa miaka sita anachukua majukumu kutoka kwa Lydia Nzomo aliyestaafu Novemba mwaka jana.

Uteuzi wa Muturi kuongoza TSC ulifanywa na rais Uhuru Kenyatta ambaye pia alimteua Timon Oyucho kuhudumu kama mwanachama wa tume huyo kwa miaka sita.

Hadi kuteuliwa kwake, Oyucho amekuwa wakili wa tume hiyo ya TSC.