Serikali ya Kenya imeondoa vikwazo kwa wawekezaji kutoka Tanzania wanaopania kufanya biashara hapa nchini.

Akizungumza alipohudhuria mkutano na wafanyibiashara kutoka sekta ya kibinafsi jijini Nairobi, rais Uhuru Kenyatta amesema wawekezaji hao wako huru kufanya biashara nchini bila kuwa na vibali au visa.

Rais Kenyatta vile vile amewaagiza mawaziri husika kuondoa msongamano wa matrela kwenye mpaka wa Namanga ili kuruhusu biashara kuendelea baina ya Kenya na Tanzania.

Kwa upande wake rais Samia Suluhu akihutubu kwenye kongamano hilo amesema Tanzania ipo radhi kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya na kwamba milango yake iko wazi kwao kufanya biashara.

Baadaye alasiri hii rais huyo wa taifa jirani atahutubia kikao cha pamoja cha bunge akiwa ni rais wa tatu kupata fursa hiyo adimu.