Hii leo Kenya inajiunga na ulimwengu kusherehelea siku ya uhuru wa wanahabari duniani.

Siku hii ilitengwa kuikumbusha serikali za mataifa mbalimbali ulimwenguni kujitolea kwao kueshimu uhuru wa wanahabari.

Victor Bwire kutoka shirika la wanahabari nchini MCK anasema wanahabari humu nchini wamejikakamua kuwapasha habari wakenya licha ya kuwepo kwa janga la corona.

Hata hivyo Bwire anasema licha ya kujitolea kwa wanahabari, wengi wameathirika na janga la corona kutokana na kukatwa mishahara na wengine hata kuachishwa kazi.

Bwire anatoa wito kwa washikadau kushikana mikono kutetea maslahi ya wanahabri nchini na kupinga sheria ambazo zinawaathiri wanahabari katika kazi zao.

Ulimwenguni kote, wanahabari wasiopungua thelathini waliuawa mwaka jana pekee, 21 kati yao wakilengwa kutokana na kazi zao, wengine tisa wakifariki baada ya kujipata kwenye makabiliano wakitekeza kazi zao.

Mexico, Afghanistan na Ufilipino yametajwa kuwa mataifa ambapo wanahabari hulengwa sana kutokana na kazi zao.