Naibu Rais William Ruto ameandaa kikao cha siku tatu na viongozi kutoka kaunti kumi na moja za mlima Kenya, anapojiandaa kwa kinyanganyiro cha ikulu hapo mwakani.

Kikao hicho cha wikendi nzima kilijadili uchumi wa taifa na jinsi ya kuwasaidia wafanyibiashara wadogowadogo na pia wakulima.

Mkutano huo umeonekana kuwa juhudi za naibu Rais kutafuta uungwaji mkono kutoka eneo la Mlima Kenya.

Viongozi hao pia wameripotiwa kusukuma ajenda ya eneo hilo la Mlima Kenya iwapo Dr Ruto atafanikiwa kumrithi Rais Uhuru Kenyatta kwneye uchaguzi mkuu wa Agosti mwakani.