Mzee wa miaka 60 ameponea kuchomwa na raia huko Nyeri baada ya kukutwa akiiba machungwa mchana peupe katika soko la Chaka.

Pasipokuwa na uwoga kuhusu kichapo kilichokuwa kinamuongoja, jamaa huyo alisikika akiwaambia wananchi waliojawa na hasira wamchome.

Mshukiwa alinaswa akipakia kwenye lori magunia manne ya machungwa kwa mujibu ya walioshuhudia kioja hicho.

Inaarifiwa kwamba hali ya vuta niuvute ilianza wakati wafanyibiashara walimuona mshukiwa akipakia machungwa hayo yaliyokuwa yameachwa na mwenyewe ambaye hakuwa karibu.

Kilichomuokoa mshukiwa ni vilio vya akina mama walioomba asemehewe na wakamuonya asurudie tabia hiyo tena.