Watu 19 zaidi wamefariki baada ya kuambukizwa virusi vya corona na kufikisha idadi ya maafa yaliyotokana na virusi hivyo kuwa 2,763.

Wizara ya Afya inasema kati ya wagonjwa 1,298 waliolazwa kwenye hospitali mbalimbali wakipokea matiabbu ya corona, 190 kati yao wako kwenye chumba cha watu mahututi huku wengine 6,652 wakiendelea kupokea matibabu kutoka nyumbani.

Idadi ya watu walio na virusi hivyo imepanda na kufikia 160,422 baada ya wengine 369 zaidi kupatwa na corona kutoka kwa sampuli 4,469 zilizopimwa hivi punde zaidi.

Kiwango cha maambukizi nchini sasa asilimia 8.3, siku moja tu baada ya Rais Uhuru Kenyatta kufungua mipaka ya kaunti tano zilizofungwa.

Watu 72 zaidi wamepona baada ya kudhibitishwa kuambukizwa virusi hivyo na kufikisha idadi ya waliopona nchini kuwa 108,861.