Idara ya polisi imebuni kikosi maalum kuchunguza utekaji nyara na mauaji ya wanaume wanne kutoka Kitengela siku tisa zilizopita.

Inspekta mkuu wa poliisi Hillary Mutyambai anasema kikosi hicho tayari kimeanza kazi na kuwahaidi wakenya kuwa kwa muda wa mwezi mmoja, watapata majibu hivi karibuni kuhusiana na mauaji hayo ya kutamausha.

Wanne hao Jack Onyango, Elijah Obuong, Benjamin Mbai na Brian Oduor wanaripotiwa kutoweka muda mfupi baada ya kushiriki mlo pamoja.

Tayari miili inayoaminika kuwa ya Onyango, Obuong na Mbai imepatikana huku kikosi hicho kikiendelea kumtafuta aliko Oduor.

Hata hivyo familia ya Onyango imekana kuwa mwili uliopatikana jana katika mto Mathioya si ule wa jamaa wao.