Naibu mwenyekiti wa chama cha Jubilee David Murathe amefika mbele ya kamati ya bunge inayochunguza sakata ya kupotea kwa pesa za corona katika shirika la kununua vifaa vya matibabu KEMSA.

Kwenye kikao kilichokumbwa na malumbano, Murathe amejitetea dhidi ya madai kuwa alipewa kandarasi kutoka kwa KEMSA kusambaza vifaa vya matibabu pasipo kufuatwa kwa sheria.

Akirejelea kampuni anayohusishwa nayo ya Kilig kwenye sakata hiyo, Murathe amejiondoa lawamani huku akiwahusisha wendani wa naibu rais William Ruto na umiliki wa kampuni hiyo.

Murathe ameshikilia kwamba yeye sio mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo inayodaiwa kupewa kandarasi wa Shilingi bilioni nne kusambaza vifaa vya matibabu kwa KEMSA.