Mtoto wa siku 14 ni miongoni mwa watu 834 walipatwa na corona katika muda muda wa saa Ishirini na nne zilizopita kati ya sampuli 8,498.

Maambukizi hayo yako katika asilimia 9.8% huku idadi ya visa hivyo nchini ikiwa 158,326 kufikia sasa.

Watu 579 zaidi wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 107,882 huku maafa 23 zaidi yakidhibitishwa na kufikisha idadi hiyo kuwa 2,688.

Kuhusu shuguhli ya utoaji chanjo ya Astrazeneca inayoendelea kote nchini, jumla ya watu 853,081 wamepata chanjo hiyo ikiwemo watu walio na umri wa miaka 58 na zaidi 494,278, wahudumu wa afya 155,294, maafisa wa usalama 71,604, walimu 131,905.