Kamati ya pamoja ya bunge kuhusu haki na maswala ya kisheria (JLAC) kwa kauli moja imependekeza kupitishwa kwa mswada wa marekebisho ya katiba BBI bila kufanyiwa marekebisho.

Naibu mwenyekiti wa kamati hiyo na mbunge wa Rarieda Otiende Amollo ameliambia bunge kwamba hawana jukumu la kurekebisha mswada huo kwa sababu umeidhinishwa na wananchi.

Ameongeza kuwa kamati hiyo ilikubaliana kwamba hatma ya mswada huo inasalia na wananchi watakaofanya uamuzi wa mwisho kupitia kura ya maamuzi.

Hata hivyo katika bunge la senate mambo ni tofauti kwani mwenyekiti wa kamati ya bunge hilo kuhusu maswala ya kisheria Okong’o Omogeni amesema wanafaa kupewa nafasi ya kurekebisha dosari zilizogunduliwa kwenye ripoti hiyo.