Rais Uhuru Kenyatta amewasilisha rasmi jina la Martha Koome kusailiwa kabla ya kuapishwa rasmi kuwa Jaji Mkuu.
Bunge lina muda wa siku 28 kumpiga msasa Koome na kuwasilisha ripoti yake bungeni kwa mjadala.
Spika wa bunge la kitaifa Justine Muturi amedhibitisha kupokea jina la Martha Koome aliyependekezwa kumrithi David Maraga kwa wadhifa wa Jaji Mkuu kuambatana na sehemu ya mia moja na sitini na sita 166 ya katiba.
Kwenye taarifa kukabirisha uteuzi wake, jaji Martha Koome ameihongera tume ya huduma za mahakama JSC kwa kumuidhinisha licha ya ushindani mkali.
Jaji Koome amesema itakuwa mi heshima kubwa kwake kutumikia nchi ya Kenya kama Jaji Mkuu iwapo ataidhinishwa
Hayo yakijiri
Baraza la magavana limempongeza jaji Martha Koome kwa uteuzi wake kuwa Jaji Mkuu.
Magavana wamemtaja Koome kama mtu aliye na uzoefu katika maswala ya kisheria na mtetezi wa haki za kibinadamu.
Baraza hilo limeeleza kuwa uteuzi huo ni wa kuwa wa kihistoria, ikizingatiwa kwamba yeye ni mwanamke wa kwanza kuteuliwa nchini kwa wadhifa huo.
Waliohojiwa kumrithi David Maraga aliyestaafu ni pamoja rais wa mahakama ya rufaa William Ouko, Juma Chitembwe, David Marete, mawakili Fred Ngatia na Philip Murgor pamoja na wasomi wa maswala ya kisheria Profesa Kameri Mbote na Dr. Dr. Moni Wekesa.