Bunge la kaunti ya Wajir limepiga kura ya kumuondoa gavana Mohamed Mohamud Abdi licha ya kuwepo kwa agizo la mahakama linalozuia mjadala huo.

Madiwani 37 walipiga kura kuunga mkono hoja hiyo huku 10 wakipiga kura ya kupinga.

Madiwani wawili hawakuwepo kushiriki kwenye mjadala huo.

Gavana huyo anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo utumizi mbaya wa mamlaka na ufisadi.