Watu 7 watahojiwa kwa wadhifa wa jaji wa mahakama ya upeo kujaza pengo lililoachwa na Jacktone Ojwang’ aliyestaafu.

Watakaohojiwa ni pamoja na majaji Said Juma Chitembwe, Marete Njagi, Nduma Nderi, William Ouko, Joseph Sergon pamoja na mawakili Alice Yano na Dkt. Lumumba Nyaberi.

Tume ya huduma za mahakama JSC imeratibiwa kuendesha mahojiano hayo kati ya Jumatatu na Alhamisi wiki ijayo.

Jaji Martha Koome alikuwa ameorodheshwa kuhojiwa ila jina lake limeondolewa kwa sababu ameteuliwa kwa wadhifa wa Jaji Mkuu huku jaji M’inoti Kathurima akijiondoa.