Abiria wanaotumia  magari yanayohudumu katika kituo cha magari cha Railways wamelazimika kutembea  kutoka kituo kipya cha magari cha Greenpark baada ya  Mamlaka ya usimamizi wa Nairobi NMS hii leo kufanya majaribio ya kuondoa matatu katikati mwa jiji.

Baadhi ya abiria wamelalama kutojua kuhusu mabadiliko hayo pamoja  na kuchukua muda mwingi kufika katikati mwa jiji.

Hata hivyo wengine wamefurahia mabadiliko hayo wakisema yanalenga kupunguza msongamano wa magari jijini.

Kwa upande wao madereva wa magari ya uchukuzi wa umma wamelalama kuhusu msongamano wa magari kabla ya kufika katika kituo hicho.

Waziri wa barabara katika shirika la NMS Michael Ochieng amesema majaribio hayo yamefaulu na kusema baadhi ya changamoto wamelazimika kushughulikia ni kutafuta mabasi maalum ya kuwabeba watu walio na mahitaji maalum hadi katikati mwa jiji.