Serikali imezindua kampeni ya kusambaza neti za kuzuia mbu wanaoambukiza malaria million 15.7 katika kaunti 27 ambazo zinashuhudiwa idadi kubwa ya wagonjwa wa malaria.

Katibu mwandamizi kaika wizara ya Afya Rashid Aman anasema kampeni hiyo itaigharimu serikali shilingi billion nane huku wakenya million 25 wakilengwa.

Aman anasema taifa la Kenya limepiga hatua kubwa katika kupambana na ugonjwa huo kwani kiwango cha maambukizi kimeshuka kutoka asilimia 8 mwaka 2015 hadi asilimia 5.6 mwaka huu.

Mwenyekiti wa jopo la kusimamia chanjo Willis Akhwale anasema malaria huua takribani wakenya elfu ishirini kila mwaka.

Wawili hao walikuwa wanazungumza jana wakati Kenya ilijiunga na ulimwengu kuadhimisha siku ya malaria duniani.