Mashirika mbalimbali ya kutetea haki za kibinadamu yanataka dhulma za kinyumbani kutangazwa kuwa janga la kitaifa.

Yakiongozwa na shirika la Haki Afrika, mashirika hayo yanadai kuwa asilimia tisini (90%) ya wanaotekelza matendo hayo ni wanaume ambao ni ndugu wa karibu.

Mashirika hayo yanahoji kuwa hata maafisa wa usalama ambao wanafaa kuaminiwa na usalama wa raia wa kawaida wanatekeleza matendo hayo.

Haya yanajiri siku moja baada ya ripoti kuonesha kwamba visa vya dhulma za kimapenzi viliongezeka kwa asilimia 92% kati ya mwezi Januari na Juni mwaka jana.

Unywaji wa pombe, utumizi wa dawa za kulevya, kuzorota kwa maadili, mizozo ya kinyumbani na malezi hafifu kama baadhi ya sababu zinazochangia kuongezeka kwa visa hivyo.

Utafiti uliofanywa na kituo cha uhalifu wa kitaifa ambao umetaja kaunti za Nairobi, Kakamega, Kisumu, Nakuru na Kiambu kama zinaongoza kwa kurekodi idadi kubwa ya visa hivyo.