Gavana wa Kisumu Profesa Peter Anyang Nyong’o ameitwa kufika mbele ya bunge la Senate Ijumaa ijayo kujibu maswali kuhusu matumizi ya pesa za kupambana na janga la corona.

Profesa Nyong’o ametakiwa kufika mbele ya kamati ya bunge la Senate kuhusu afya kuhojiwa baada ya kufeli kufanya hivyo Jumanne iliyopita.

Kamati hiyo imemtaka gavana huyo kufika mbele yake Ijumaa ijayo Aprili 30.

Aidha Profesa Nyong’o ameagizwa kutuma stakabadhi zote anazopania kutumia kufikia Jumatano wiki ijayo.

Iwapo atakosa kufika kwa mara nyingine, kamati hiyo itatumia kanuni zake kumtoza faini ya Sh500,000 au iagize ashikwe.