Wanaume watatu wamesumkwa jela miaka 15 baada ya kupatwa na hatia ya kumbaka kwa zamu msichana,15, aliyekuwa mja mzito.

Miongoni mwao ni mpenziwe,19, aliyekuwa katika kidato cha nne wakati wa tukio hilo Machi 28, 2020 kwenye soko la Mulango, Tigania ya kati kaunti ya Meru.

Timothy Muli,20, Duncan Mwirigi,22, na mpenziwe msichana huyo walimkuta msichana akiwa amejikinga kutokana na mvua kubwa iliyokuwa inanyesha na kuahidi kumsaidia.

Hata hivyo walimfunga mikono na mdomo na kisha kumpeleka kwa nyumba ya Mwirigi ambapo walimbaka kwa zamu na kisha kumtupa nje aendelea kunyeshewa na mvua.

Msichana alitafuta hifadhi kwa mmoja wa rafiki zake wa kike ambapo wazazi wake waliripoti tukio hilo kwa Polisi ambaye baadaye uchunguzi wa matibabu ulibaini kwamba alikuwa na mimba.