Mwili wa Antipas Nyanjwa, naibu mkurugenzi wa uchunguzi katika tume ya ardhi nchini (NLC) utafanyiwa upasuaji leo (Alhamisi).

Mtalaamu huyo wa uchunguzi alifariki Jumatatu baada ya kuripotiwa kupatwa na matatizo ya kupumua alipokuwa anakula chakula cha mchana katika mkahawa mmoja kwenye barabara ya Ngong.

Juhudi za kumkimbiza hospitalini kwa matibabu ya haraka ziliambulia patupu kwani alifariki pindi alipofikishwa katika hospitali ya Coptic.

Rafikize wanasema alikuwa amerejea kazini baada ya kupona ugonjwa wa corona.

Kifo chake kinakuja mwezi mmoja baada ya mkurugenzi wa mawasiliano katika tume hiyo ya ardhi kuuawa katika hali ya kutatanisha.