Chama cha UDA kinachohusishwa na naibu Rais William Ruto kimeomba muda zaidi kusuluhisha tofauti baina yake na chama tawala cha Jubilee.

Katika barua kwa msajili wa mahakama baada ya Jubilee kuomba talaka ya makubaliano yaliyoafikiwa mwezi Mei mwaka elfu mbili kumi na nane, katibu mkuu wa UDA  Veronica Maina amesema wataelekea kwa jopo la kutatua migogoro ya vyama vya kisiasa ili kutafuta suluhu.

Chama hicho ambacho awali kilifahamika kama PDR kimeomba msajili wa vyama vya kisiasa Ann Nderitu kutoidhinisha ombi la Jubilee kukatisha uhusiano baina yao hadi pale jopo hilo litakapotoa uamuzi wake.

Chama hicho pia kinataka Nderitu kuzuia Jubilee kumngatua naibu kiongozi wa wengi katika bunge la seneti, seneta Fatuma Dullo hadi pale mchakatao wa kutafuta suluhu utakapomalizika.

Katibu mkuu wa Jubilee Raphael Tuju aliandikia afisi ya msajili wa vyama vya kisiasa akiomba talaka baina yao na UDR kwa msingi kuwa chama hicho kimevunja makubaliano baina yao.