Rais Uhuru Kenyatta yuko mjini Kinshasa, DRC kwa ziara rasmi ya siku tatu kwa mwaliko wa mwenyeji wake rais Felix Tshisekedi.

Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa karibu baina ya mataifa haya mawili kupitia Biashara na utangamano wa raia wake.

Mengine yatakayopewa kipau mbele wakati wa ziara hiyo ni uhusiano wa kidiplomasia baina ya Kenya na Congo sawa na kushirikiana katika maswala ya usalama.

Kenya na DRC yanaunganishwa na lugha ya Kiswahili ambayo huzungumzwa Mashariki mwa taifa hilo.