Rais Uhuru Kenyatta anatazamiwa kukabidhiwa majina ya watakaokuwa kwenye jopo litalokuwa na jukumu la kuwatafuta makamishna wapya wa tume ya uchaguzi a mipaka (IEBC).
Tume ya huduma za bunge PSC inayoongozwa na spika wa bunge la kitaifa Justine Muturi inatazamiwa kumkabidhi rais orodha hiyo kwa uteuzi kabla ya kuanza rasmi mchakato wa kuwasaka makamishna wapya.
Jopo hilo linafaa kuwa wanaume na wanawake wawili kutoka PSC, mwakilishi mmoja wa chama cha Mawakili nchini (LSK) na wawakilishi wawili wa makundi ya kidini.
Hatua hii inakuja baada ya rais Kenyatta kutangaza wazi nafasi za makamishna wanne waliojiuzulu baadhi yao wakizawadiwa kazi za serikali.
Nafasi hizo zilisalia wazi kufuatia kujiuzulu kwa makamishna Consolata Nkatha, Paul Kurgat, Roselyne Akombe na Margaret Mwachanya.