Naibu rais William Ruto amepuuzilia mbali uwezekano wa kubuni muungano wa kisiasa kati yake na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga.

Ruto akihojiwa na kituo cha televisheni cha Citizen amesema anatarajia kushindana na Odinga kwenye kinyanganyiro cha kuwania urais 2022 kwa sababu waziri huyo mkuu wa zamani ndiye ana uwezo wa kumenyana naye.

Ruto vile vile amesema hajashiriki kwenye mazungumzo yoyote ya kushirikiana kisiasa na Odinga akisema mashauriano baina yake na naibu kiongozi wa chama cha ODM Wycliffe Oparanya yalijikita kwenye siasa zake za walala hoi.

Kuhusu ushirikiano baina yake na rais Uhuru Kenyatta, Ruto ameashiria kwamba ndoa yao iliingia doa waliposhinda awamu ya pili ambapo rais alionekana kumtenga.

Amesema iwapo itakuwa vigumu kusalia katika chama chama cha Jubilee, basi yeye na wendani wake hawatakuwa na budi ili kujiunga rasmi na chama cha United Democratic Alliance (UDA).