Mwanaharakati mmoja amewasilisha kesi katika mahakama ya Milimani akitaka shughuli nzima ya kumteua Jaji Mkuu inayoendelea kusimamishwa mara moja.

Kwenye kesi yake, mlalamishi Memba Ocharo kupitia kwa wakili wake Danstan Omari anahoji kuwa baadhi ya wanaowania wadhifa wa Jaji Mkuu hawajatangaza wazi mali yao kwa umma kwa mujibu wa katiba.

Mwanaharakati huyo vile vile anapinga jopo linaloendesha mahojiano hayo kuongozwa na Olive Mugenda akisema kwa mujibu wa sheria, naibu jaji mkuu Philomena Mwilu ndiye anapaswa kuwa mwenyekiti.

Mahojiano hayo yameingia siku yake ya tano huku wakili Philip Murgor akihojiwa.

Wengine ambao wamehojiwa kwa wadhifa huo ni; Said Juma Chitembwe, Profesa Patricia Kameri Mbote, Martha Koome Karambu na David Marete Njagi.