Shule zitafunguliwa kwa muhula wa tatu tarehe 10 mwezi Mei kama ilivyopangwa kwa kuzingatia hali ya ugonjwa wa corona nchini.
Waziri wa elimu Profesa George Magoha ameelezea matumaini yake kwamba msambao wa virusi hivyo haitavuruga kalenda ya masomo na kuwaagiza wakuu wote wa elimu kuhakikisha kuwa wanapuliza dawa katika shule kabla ya shule kufunguliwa.
Profesa Magoha vile vile amedokeza kwamba shughuli ya kuwateua watahiniwa watakaojiunga na kidato cha kwanza itafanyika Mei 28, 2021 huku akitoa hakikisho watahiniwa wote waliokalia mtihani wa darasa la nne KCPE watajiunga na shule ya upili.
Wanafunzi 9,000 watapata ufadhili wa masomo chini ya mpango wa Elimu unaotolewa na serikali.