Faith Mumo wa shule ya Karimwailu kaunti ya Makueni ndiye mwanafunzi bora katika mtihani wa darasa la nane (KCPE) mwaka huu akiwa na alama 433.

Akitangaza matokeo rasmi ya mtihani huo, waziri wa elimu Profesa George Magoha amesema kwamba Wesonga Nanzala wa shule ya Wasichna ya Chogoria na Muriithi Gakenia wa shule ya wasichana ya Maseno wameibuka wa pili kwa kupata alama 432.

Kwa mujibu wa Profesa Magoha, shule za umma kwa mara nyingine zimefanya vyema ikilinganishwa na shule za kibinafsi kwenye mtihani huo.

Wanyonyi Makhanu wa shule ya Nzoia ameibuka wa nne na alama 431 sawa na Castro Williams wa shule ya kibinafsi Crystal Hill Academy.

Aidha, waziri Magoha wanafunzi wa kike wameongoza kwa kufanya vyema katika masomo ya Kiingereza, Kiswahili na somo la iIhara ikilinganishwa na wenzao wa kiume ambao wameongoza katika masomo ya Hesabu, Sayansi na somo la kijamii na dini.