Polisi wa kukabiliana na ugaidi wanawazuilia mama na bintiye baada ya kushikwa wakiwa na silaha nyumbani kwao Racecourse, Dagoretti Corner, Nairobi.

Washukiwa Goretti Mwihia na mwanawe Joyce Mwihia wenye uraia wa mataifa mawili walipatikana na silaha hizo ikiwemo bunduki, bastola nne na risasi 3,700.

Maafisa wa usalama wanaamini kwamba silaha hizo ziliingizwa nchini kisiri na makusudi ya kutekeleza ugaidi.

Wawili hao wanashikiliwa na Polisi wakihojiwa wakisubiri kufikishwa mahakamani.