Waziri wa elimu Profesa George Magoha anatarajiwa kutangaza matokeo ya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE wakati wowote.
Profesa Magoha anakutana na Rais Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya rais kumkabidhi matokeo ya KCPE ya mwaka 2020 kabla ya kutangaza rasmi.
Mtihani wa KCPE uliokuwa ufanyike Novemba mwaka jana ila ukafanyika mwaka huu kutokana na janga la covid-19 lililotatiza kalenda ya masomo baada ya kufungwa kwa shule.
Watahiniwa zaidi ya Milioni moja walikalia mtihani huo kati ya Machi 22 na 24.
Katibu mkuu katika wizara ya elimu Dkt. Julius Jwan amenukuliwa akisema kwa watahiniwa hao watajiunga na kidato cha kwanza Julai mwaka huu.
Aidha zaidi ya watahiniwa 200 waliokuwa wajawazito walifaulu kukalia mtihani huo kati ya 3,500 waliopata uja uzito kabla ya mtihani huo.