Lawrence Warunge,22, mshukiwa mkuu wa mauji ya familia yake katika eneo la Kiambaa, kaunti ya Kiambu atakabiliwa na mashtaka matano ya mauji.

Hii ni baada ya kukamilika kwa muda uliotengwa kwa mshukiwa huyo kufanyiwa uchunguzi wa kiakili.

Ripoti kutoka katika hospitali ya Mathari inaonesha kwamba Warunge ana akili timamu na hivyo tayari kushtakiwa kwa mauji.

Mshukiwa anadaiwa kuwaua babake Nicholas Warunge, mamake Anne Wanjiku, kakake, binamuye pamoja na mfanyikazi wao James Kinyanjui mapema mwaka huu.

Mshukiwa wa pili, Sarah Muthoni ambaye ni mpenzi wake Warunge aliachiliwa huru kwa dhamana na atakuwa shahidi wa upande wa mashtaka.