Wakenya wamepata afueni ya muda baada ya serikali kusalimu amri na kukosa kuongeza bei za mafuta.

Kinyume na ilivyotarajiwa, tume ya kudhibiti kawi nchini EPRA imetangaza kuwa bei za mafuta hazitabadilika kwa muda wa mwezi mmoja ujao na zitasalia zilivyo tangu mwezi jana.

Hii ina maana kwamba Petroli jijini Nairobi itasalia kuuzwa kwa Sh122.81 kwa kila lita, Diseli itapatikana kwa Sh107.66 na mafuta taa kwa Sh97.85.

Mjini Mombasa, Petroli itauzwa Sh120.41, Diseli Sh105.27 na mafuta taa Sh95.46.

Lita moja ya Petroli mjini Nakuru itauzwa kwa Sh122.44, Diseli Sh107.55 na mafuta taa Sh97.96.

Eldoret Petroli itapatikana kwa Sh123.36, Diseli kwa Sh108.46 na mafuta taa 98.68. Wakaazi wa Kisumu watanunua Petroli kwa Sh123.36, Diseli kwa Sh108.46 na mafuta taa kwa Sh98.68.