Wakenya watarajie bei za mafuta kupanda zaidi wakati tume ya kudhibiti kawi nchini EPRA itakapotangaza bei mpya Jumatano.

EPRA inatarajiwa kutangaza bei zitakazotumika kwa muda wa mwezi mmoja ujao baada ya kuongeza bei hizo mwezi uliopita na kusababisha ghadhabu miongoni mwa Wakenya.

Bei ya Petroli inatazamiwa kuongezeka kwa Sh4.30 na hivyo kuuzwa kwa Sh127.11 kwa kila lita jijini Nairobi.

Bei ya Diseli inatarajiwa kuongezeka kutoka Sh107.66 hadi Sh109.96 kwa lita moja.

Kwenye bei zilizotangazwa na EPRA mwezi uliopita, mafuta ya Petroli yaliongzeka kwa shilingi 7.63, Diseli kwa shilingi 5.75 na mafuta taa yakiongezeka kwa shilingi 5.41.